Ligi KuuNyumbani

Ihefu, Ruvu mtihani Ligi Kuu leo

KLABU za Ihefu na Ruvu Shooting leo zitakuwa kwenye mtihani zitakaposhuka viwanja tofauti katika mfululizo wa Ligi Kuu ya soka Tanznaia Bara.

Ihefu ni mwenyeji wa Mtibwa Sugar kwenye uwanja Highland Estates uliopo Mbarali mkoani Mbeya.

Mtibwa Sugar inashika nafasi ya 5 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 24 baada ya michezo 17 wakati Ihefu ipo nafasi ya 14 ikiwa na pointi 14 baada ya michezo 17 pia.

Nayo RUvu Shooting itaikaribisha Namungo kwenye uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Namungo ipo nafasi ya 9 ikiwa pointi 22 baada ya michezo 17 wakati Ruvu Shooting inashika nafasi ya 15 ikiwa na pointi 12 baada ya michezo 17 pia.

Related Articles

Back to top button