Heidenheim yang’ang’ana Bundesliga

ELVERSBERG:KLABU ya Heidenheim imefanikiwa kubaki katika ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga, baada ya bao la dakika za usiku la Leo Scienza kuzima ndoto za klabu ya Bundesliga 2 ya Elversberg katika mchezo wa mkondo wa pili wa ‘playoff’ uliopigwa Jumatatu usiku baada ya bao lake kufanya ubao wa matokeo kusoma 2-1 ndani ya dakika za nyongeza.
Heidenheim Waliomaliza katika nafasi ya 16 kwenye Bundesliga msimu huu wamefanikiwa kupata ushindi huo muhimu ugenini dhidi ya Elversberg ambao hawajawahi kucheza ligi ya Bundesliga baada ya mchezo wa awali nyumbani kwa Heidenheim kumalizika kwa sare ya 2-2 hivyo kubaki Bundesliga kwa jumla ya mabao 4-3.
Licha ya kuumiliki mchezo huo kwa kiwango kikubwa, Elversberg walishindwa kutoboa safu bora ya ulinzi ya Heidenheim na ndoto yao ya kucheza Bundesliga kwa mara ya kwanza iliota mbawa baada ya Scienza kushindilia bao safi ndani ya dakika tano za nyongeza bao lililoibua shangwe kwa wageni hao.
Baada ya ushindi huo Heidenheim sasa watacheza msimu wao wa pili wa Bundesliga wakati VfL Bochum na Holstein Kiel walishuka daraja moja kwa moja. FC Cologne na Hamburg SV wamepanda moja kwa moja kucheza msimu ujao wa Bundesliga