‘Hakuna rushwa ya ngono kwenye urembo’
DAR ES SALAAM: Miss Tanzania 2023, Halima Kopwe amefichua siri iliyofichwa kuhusu rushwa ya ngono kwenye mashindano ya kusaka warembo hasa wanapokuwa kambini na kuomba warembo kuheshimiwa.
Akizungumza na Spotileo leo jijini Dar es Salaam Halima amesema kuwa watanzania wanatakiwa kujua kuwa urembo ni heshima na watu waachane na maneno ya mitandaoni.
“Nimekuwa Miss Tanzania nilipita kanda, wilaya, mkoa, Taifa hadi Duniani lakini sijawahi kuona kitu kama hicho ninachojua warembo wanapokuwa kambini wanaishi kwa heshima na ulinzi pasipo kuonana na ndugu, jamaa wala marafiki.
“Na wasichokijua watanzania ni kuwa kambini warembo tunafundishwa vitu vingi ikiwemo usafi binafsi, usafi wa mazingira na jinsi ya kuongea unatakiwa ‘kuposti’ nini nini ‘usiposti’ kutunza ngozi na vitu vingi vizuri jinsi ya kula kutembea.
“Siri mnatyosema inafichwa sijui kuhusu watu kuja kuwachukua warembo kutoka nao hakuna na kama ingekuwepo nisingesita kusema ningesema ili kuokoa wengine.
Alipoulizwa kuhusu wadhamini kutoa mfano gari na kujichagulia mrembo wa kuondoka nae kutokana na ukubwa wa zawadi aliyotoa amefafanua.
“Nimekuwa Miss Tanzania na sasa ni Mwaandaji wa Shindano la kusaka warembo kweli kuna shida ya wadhamini kujitokeza lakini hata wanaojitokeza hawawezi na hawafanyi hivyo kwa kuwa amekuja kusapoti shindano sio mshiriki.”amesema Halima
Pia ameongeza kuwa mashindano ya urembo bado hayajapewa thamani na hadhi inayotakiwa ni wakati wa makampuni mbalimbali kujitokeza na kudhamini mashindano haya.
“Niombe serikali na makampuni binafsi kujitokeza kudhamini mashindano haya yatakayoleta mabadiliko zaidi katika sekta ya urembo na kuwafanya warembo kujikita katika kurudisha zaidi kwenye jamii kila wanachonufaika nacho.”ameongeza Halima