Tetesi
Gerrard afikiriwa mchongo Leeds

BAADA ya kutimuliwa Aston Villa Oktoba 21, 2022, klabu ya Leeds United inafikiria kumpa ajira Steven Gerrard.
Mwingereza mwenzake Scott Parker baada ya kufukuzwa Fulham na Bournemouth naye anatajwa kwenye orodha ya kuifundisha Villa.
Mtandao wa Telegraph pia umeeleza kocha wa zamani wa West Bromwich Albion, Carlos Corberan pia anatajwa kwenye orodha hiyo.
Makocha hao wanawania nafasi ya kuifundisha timu hiyo, baada ya Sam Allardyce kutimuliwa jana kwa kushindwa kuinusuru Leeds kushuka daraja.