Gamondi acha hizo wewe!

DAR ES SALAAM: Kocha wa @yangasc, Miguel Gamondi ni kama ameweka mtego kwa wapinzani wake baada ya leo kusema kwamba mbio za ubingwa bado sana huku akizitaja @simbasctanzania na @azamfcofficial kama timu tishio katika mbio za ubingwa.
Akizungumzia maandalizi ya mchezo wa kesho dhidi ya @kagerasugarfcofficial, Gamondi amesema hawezi kuwakosea heshima wapinzani kwa kusema mbio za ubingwa zimemalizika wakati kila timu bado ina michezo iliyosalia hivyo lolote linaweza kutokea.
Kocha huyo wa Kimataifa wa Argentina ameongeza kuwa anaingia kwenye mchezo wa kesho kuzisaka alama tatu ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kuwa mabingwa licha ya kwamba anafahamu utakuwa mchezo mgumu.
Ikumbukwe tofauti ya alama kati ya Yanga na makamu vinara Azam FC ni alama nane huku kila timu ikisaliwa na michezo mitano tu na dadili zinaonekana kuwa Yanga wana nafasi kubwa ya kwua wabingwa lakini Gamondi amebadili upepo na kufuata njiaz ake.
Mchezo wa Yanga Vs Kagera Sugar utakaopigwa kesho jioni Uwanja wa Azam Complex Chamazi ni moja ya michezo ya maamuzi kwenye mbio za ubingwa kwani kama Yanga wakishinda watabakiza alama 5 tu kutetea ubingwa wa ligi kwa mara ya tatu.