Gamond ajibebesha lawama
DAR ES SALAAM: BAADA ya kupoteza mechi mbili mfululizo za Ligi Kuu Tanzania Bara, Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema atazibeba lawama kama kiongozi wa benchi la ufundi.
Yanga imepoteza mechi dhidi ya Azam FC na jana usiku walikubali kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa walima asali, Tabora United uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi Dar es Salaam.
Gamondi amesema amekubali matokeo na hakuna mchezaji wa kulaumiwa zaidi yake , kilichowapa ushindi Tabora United sio motisha bali hamu ya wachezaji kusafisha matokeo mabaya waliyoyapata kwenye mechi za nyuma.
“Tulitengeneza nafasi hazikutumika mfano Kennedy Musonda, siwezi kulaumu Wachezaji ila tazama pia ratiba yetu tuna mechi sita ndani ya siku 20 na bado kalenda ya kimataifa. Wachezaji wanasafiri nchi mbili hadi tatu, wakirudi ni kama tunaanza upya” amesema kocha huyo.