
KLABU ya Mashujaa imetangaza kumsajili mshambuliaji Abdulnasir Asaa Mohamed (Gamal) kutoka Mlandege ya Zanzibar.
Gamal ni mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Mashujaa iliyopanda daraja kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao.
“Tumeinasa saini ya Abdulnasir Asaa moh’d ( GAMAL), Rasmi atawatumikia WATANGANYIKA msimu wa 2023/2024,” imesema Mashujaa kupitia mitandao yake ya kijamii.
Akiwa Mlandege Gamal amefunga magoli manne, kutoa pasi za 9 za magoli huku akishinda Kombe la Mapinduzi.