FIFA kuzuia ujumbe wa chuki Kombe la Dunia
						Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu(FIFA) limeanzisha huduma mpya ya ulinzi ya mitandao ya kijamii inayolenga kuzuia wachezaji wa timu 32 zinazoshiriki Kombe la Dunia kupata machapisho ya chuki kwenye mitandao ya kijamii.
Kwa mujibu wa FIFA huduma hiyo itazuia wachezaji kuona ujumbe wenye matusi wanapotumia simu zao kwenye vyumba baada ya mchezo.
Kampeni dhidi ya ujumbe wenye chuki inaongozwa na kiungo wa Brazil anayekipiga Fulham, Willian Borges da Silva mwenye umri wa miaka 34 ambaye amesema alilengwa na mashabiki wakati uliopita.
“Ninaunga mkono kampeni hii kwa sababu nilikuwa Brazil mwaka mmoja uliopita, na nilikuwa nateseka sana, na familia yangu ilikuwa ikiteseka sana kwa sababu watu walianza kutushambulia kwenye mitandao ya kijamii, kushambulia familia yangu na binti zangu,” amesema Willian katika taarifa kwa vyombo vya habari.
Players from all 32 teams will have access to the service, which FIFA claims can instantly block ‘abusive, discriminatory and threatening comments’ on social media platforms.
Wachezaji wa timu zote 32 watapata huduma hiyo, ambayo FIFA inadai inaweza kuzuia papo hapo maoni ya matusi, ubaguzi na vitisho kwenye mitandao ya kijamii.
Michuano ya fainali za 22 za Kombe la Dunia inaanza Novemba 20 nchini Qatar kwa wenyeji kufungua dimba dhidi ya Ecuador katika uwanja wa Al Bayt uliopo mji wa Al Khor.
Fainali itafanyika uwanja wa Lusail ulipo mji mkuu wa Qatar, Doha Desemba 18, 2022.
				
					



