Nyumbani

Feisal asalia Azam FC kwa pesa ndefu

DAR ES SALAAM: KOCHA Mkuu wa Simba Fadlu Davids amesema mawazo yao kwa sasa yameelekea kwenye mechi ya Ngao ya Jamii ambayo kwao ni kama fainali na kipimo sahihi cha kujiandaa na michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba itacheza na Yanga Septemba 16, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam kabla ya kuelekea ugenini Botswana kuianza kampeni ya kimataifa.

Akizungumza na SpotiLeo Fadlu alisema kile kilichoonekana kwenye tamasha la Simba na mechi ya kirafiki dhidi ya Gormahia ya Kenya waliyoibuka kwa ushindi wa mabao 2-0 ni sehemu ndogo kwani moto utawaka zaidi kwenye mashindano yajayo.

“Tuna siku chache za kujiweka imara na tayari kuwakabili Yanga. Ni mchezo kama wa fainali ambao utaonesha namna tulivyo, kwa huu mwanzo nimeridhishwa sana na wachezaji. Furaha yangu kubwa ni kuona walivyocheza mbele ya mashabiki 60,000. Ilikuwa nafasi ya kukusanya taarifa muhimu na kupanga kikosi bora kwa mechi zijazo,” alisema.

Alisisitiza kuwa mashabiki waendelee kuwa na subira wakati wachezaji wakiendelea kujifunza mbinu za mfumo mpya na kuelewa namna ya kucheza bila mpira.

Aidha, kocha huyo aliongeza kuwa ameridhishwa na usajili uliofanywa na uongozi wa Simba msimu huu, akisisitiza bado anahitaji muda mfupi wa kurekebisha makosa madogo kabla ya msimu kuanza rasmi.

Kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa maandalizi ya msimu huu, Fadlu sasa atakuwa na wachezaji wake wote kamili baada ya nyota kadhaa kukosekana awali kutokana na majukumu ya timu za taifa na majeraha.

Related Articles

Back to top button