Nyumbani

Nikipata timu narudi kudaka – Kaseja

DAR ES SALAAM KIPA wa zamani wa Simba na Yanga Juma Kaseja amesema hajastaafu kucheza soka hivyo akipata timu yoyote yenye maslahi yupo tayari kurudi golini.

Kaseja ambaye kwa sasa ni kocha wa makipa katika timu ya Kagera Sugar amesema hajawahi kutangaza popote kama amestaafu soka kwa kuwa bado ana nguvu ya kucheza.

“Sijatangaza kwamba nimestaafu nikipata ofa ya kucheza timu yoyote nitacheza nguvu na ari bado ninayo ya kudaka,” amesema Kaseja.

Katika msimu uliomalizika Kagera Sugar imemaliza nafasi ya 10 na kaseja akiwa na mchango mkubwa wa udakaji kwa magolikipa wa timu hoyo.

Nafasi ya kipa inaaminiwa kuchezwa kwa muda mrefu kuliko namba za wachezaji wa ndani huku mfano mzuri ni kipa aliyedumu kwa muda mrefu Buffon.

Related Articles

Back to top button