Tetesi

Duran kukipiga na CR7 Saudia

LONDON: MSHAMBULIAJI wa Aston Villa Jhon Duran yuko mbioni kukamilisha dili la kuhamia kwenye klabu ya Al Nassr ya ligi kuu ya Saudi Arabia Saudi Pro League klabu ambayo anacheza nguli wa soka la dunia Cristiano Ronaldo.

Kwa mujibu wa BBC sport tayari makubaliano ya pande mbili yamefikiwa na ada ya uhamisho inayokadiriwa kufikia pauni milioni 65 (ambayo BBC sport hawajathibitishiwa) imekubaliwa na klabu yake na Alhamisi hii anafanyiwa vipimo vya afya tayari kujiunga na klabu hiyo.

Moja ya maafisa wa Saudi Pro League ameiambia BBC sport kuwa ikiwa atafaulu vipimo Duran atapaa kuelekea Saudi Arabia kujiunga na Al Nassr na tayari mshambuliaji huyo mwenye miaka 21 ameaga wachezaji wenzake klabuni hapo huku ikielezwa vibopa wa Al Nassr wapo London kushughulikia uhamisho huo

Alipoulizwa kuhusu kuondoka kwa Duran meneja wa Aston Villa Unai Emery alijibu ataondoka kama anataka licha ya kukiri kuwa bado anahitaji huduma ya mshambuliaji huyo.

“Ataondoka kama yeye mwenyewe anataka kuondoka, lakini mimi namtaka hapa, tuko tofauti na malengo yetu ni tofauti, naamini klabu inashughulika na hilo. Lengo letu ni kubakisha muundo wetu kwa sababu tunataka kubaki juu na labda kama tunahitaji kuuza baadhi ya wachezaji na kwakweli Sijui mpaka kila kitu itakapokamilika iwapo Duran anaondoka au la” – Amesema

Duran raia wa Colombia alijiunga na Aston Villa kutoka Chicago fire ya ligi kuu nchini Marekani kwa pauni milioni 18 na sasa anaondoka kwa dili nono linalokadiriwa kuzidi pauni milioni 64 na nyongeza. Akiwa Aston Villa amefunga mabao 12 katika mechi 29 za Mashindano yote msimu huu.

Related Articles

Back to top button