Ligi Kuu

Dodoma Jiji yajivika mabomu mechi dhidi ya Azam

DODOMA: KLABU YA Dodoma Jiji imesema haiihofii Azam kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa kesho, ikieleza tayari imeshakutana na timu zenye uwezo unaofanana na huo na kupata matokeo chanya.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo, Kocha Mkuu wa Dodoma Jiji Amani Josiah amesema anaitambua Azam kama timu bora, lakini hawana sababu ya kuiogopa kwa kuwa tayari wamecheza na timu zenye kiwango kama hicho ikiwemo Simba na Singida Black Stars na kufanikiwa kupata pointi moja.

Amesema kikosi chake kimejipanga vizuri kwa ajili ya mchezo huo dhidi ya timu ya Chamazi, huku malengo yao yakiwa ni kushinda kila mchezo wanaocheza ili kuboresha nafasi yao kwenye msimamo wa ligi.

Kuhusu kukosekana kwa beki wake Abdi Banda ambaye anatumikia adhabu ya kufungiwa, Josiah amesema ni pengo kwa timu kwa sababu ni mchezaji mzoefu, lakini ana imani wachezaji wengine waliopo wana uwezo wa kuziba nafasi yake na kuisaidia timu.

Kwa upande wa Azam FC, Kocha Msaidizi Kassim Liogope amesema wamejiandaa vizuri kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo huo.

“Dodoma Jiji ni timu inayobadilika na hivi karibuni imekuwa ikipata matokeo mazuri, hivyo naamini mchezo huo utakuwa mgumu lakini wa kuvutia,”amesema.

Related Articles

Back to top button