Diamond awapa ‘maua yao’ Zuchu, Mbosso

NYOTA wa muziki wa Bongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amewapa tano wasanii wa Lebo ya Muziki ya Wasafi (WCB) Zuhura Othman ‘Zuchu’ na Mbwana Kilungi ‘Mbosso’ kwa kuendelea kushika chati za juu kwenye muziki kitaifa na kimataifa.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Diamond alichapisha muonekano wa nyimbo mbili mmoja wa msanii Zuchu aliomshrikisha Innos B kutoka Congo ujalikanao kama Nani Remix, na wimbo wa Mbosso (Amepotea) na kuonesha kukoshwa na kazi ya wasanii hao kwa kuendelea kupasua anga, Diamond ameandika haya,
“Kwahiyo mmeamua kuwa mnapokezana wenyewe tuu hapo? Anyways Nani Remix video is out now” akimaanisha kuwa video ya wimbo huo wa Nani Remix imetoka.
Nyimbo hizo za wasanii hao zinakamata nafasi za juu kwenye nyimbo zilizovuma zaidi kwenye mitandao ya kijamii hususani Yotube.