Muziki

Demi Lee Moore atajwa Msanii wa Spotify EQUAL Africa

AFRIKA KUSINI: MWANAMUZIKI mahiri wa Afrika Kusini Demi Lee Moore ametajwa kuwa Msanii wa Spotify EQUAL Africa kwa mwezi Machi 2025, kutokana na mchango mkubwa katika muziki wa Kiafrikana.

Mpango wa EQUAL Africa wa Spotify ni kampeni ya kimataifa iliyoundwa kusaidia wanawake katika muziki kwa kuwapa elimu, msukumo, na fursa za mitandao.

Kupitia jukwaa hili, Spotify imeeleza itahakikisha wasanii wa kike wanapata mwonekano na kutambuliwa na jamii kwa mwaka mzima.

Kujumuishwa kwa Demi Lee Moore katika mpango huo kumetokana na umahiri wake katika muziki na mapokeo yake makubwa kwa mashabiki wa muziki duniani kote.

Kutajwa kuwa Msanii wa Spotify Africa ni zaidi ya heshima kwa Moore ni jukwaa la kutia moyo vizazi vijavyo. “Kuwa sehemu ya kampeni hiyo kunamaanisha ulimwengu kwangu,” Moore alielezea. “Kuwa katika nafasi ya kuhamasisha wanawake katika tasnia na wasichana wadogo wanaokua na ndoto kubwa ni baraka kubwa kwangu!”

Phiona Okumu, Mkuu wa Muziki wa Spotify kwa Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, amesisitiza umuhimu wa programu hiyo katika kuangazia wasanii wa kike wenye vipaji vikubwa.

Demi Lee Moore alivutia hisia za kitaifa kwa mara ya kwanza mwaka wa 2018 aliposhinda Die Kontrak, shindano la hadhi ya juu la muziki wa Kiafrika ambalo lilianza na zaidi ya washiriki 2,000. Ushindi wake ulimfanya kuwa maarufu, na kumruhusu kutia saini mkataba wa kurekodi na kushiriki miradi mingine mingi iliyofanikiwa ambayo iliwavutia wapenzi wa muziki wa Kiafrikana.

Related Articles

Back to top button