Tetesi

De Gea aitaka Newcastle

TETESI za usajili zinaeleza kuwa golikipa wa zamani wa Manchester United na Hispania, David de Gea,33, yupo tayari kujiunga na Newcastle United wakati The Magpies hao wakifikiria kumsajili mchezaji huyo kuzipa pengo la mlinda lango majeruhi Nick Pope,31. (Telegraph – subscription required)

Golikipa mwenzake na Pope wa timu ya taifa England, Aaron Ramsdale pia anafikiria kuhamia Newcastle, lakini The Magpies wanasita kukubali na thamani ya golikipa huyo wa Arsenal,25, ya pauni milioni 50. (Talksport)

Kocha Erik ten Hag anapigania kurejesha sapoti ya baadhi ya wachezaji wake wa Manchester United baada ya kupokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Newcastle katika mchezo wa Ligi Kuu England.(ESPN)

Wachezaji wa Manchester United wanasemekana kuhoji staili ya uchezaji ya Ten Hag na jinsi anavyomtendea winga wa England, Jadon Sancho,23.(Sky Sports)

Arsenal inakusudia kusikiliza ofa kutoka klabu nyingine kumsajili mshambuliaji wa England, Eddie Nketiah,24, Januari 2024.(Football Transfers)

Chelsea na Manchester City zinaonesha nia kuwasajili wachezaji wa River Plate, kiungo Claudio Echeverri(17), mshambuliaji Agustin Ruberto (17) na winga Ian Subiabre (16), ambao wote wameonesha kiwango kikubwa timu ya taifa ya Argentina iliyoshiriki fainali za Kombe la dunia za U17 zilizomalizika Indonesia hivi karibuni.(90Min)

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button