Tetesi

Hojlund akamilisha vipimo vya afya United

Mshambuliaji Rasmus Hojlund amekamilisha vipimo vya afya jana na sehemu ya kwanza ya utambulisho kama mchezaji mpya wa Manchester United akitokea Atalanta.

Mdenimaki huyo, 20, ameondoka katika uwanja wa mazoezi wa Carrington Manchester pamoja na uongozi wake mara baada ya kukamilisha vipimo hivyo.

Kwa mujibu wa mwandishi habari za michezo kutoka Italia, Fabrizio Romano ameeleza nyaraka rasmi za mkataba wake zitakamilishwa Jumatano wiki hii.

Ameeleza kuwa Manchester United itatoa taarifa za usajili wa mchezaji huyo muda wowote kuanzia sasa.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button