Kikapu

Dar City mambo safi Kenya

TIMU ya kikapu ya Dar City imeanza vyema mchezo wa kwanza michuano ya kanda ya tano Afrika Mashariki (EABGC) baada ya kushinda dhidi ya Equity benki ya Kenya kwa pointi 83 kwa 64.

Michuano hiyo ilianza jana na itaendelea hadi Jumamosi ya wiki hii kutafuta bingwa atakayeenda hatua nyingine za michuano hiyo kuwania nafasi ya kushiriki mashindano ya Afrika.

Kikosi hicho kinachoongozwa na nguli wa kimataifa wa mchezo huo Hasheem Thabeet kiliwakilisha vizuri.

Msemaji wa Dar City Revocatus Chipando ‘Baba Levo’ amewataka watanzania kusherehekea ushindi huo akisema wamemuwakilisha vema Rais Samia Suluhusu Hassan.

“Tuko hapa Nairobi Kenya, tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan tunakuwakilisha vyema, Dar City itaendelea kupeperusha vyema bendera ya nchi,”amesema.

Mwakilishi mwingine wa Tanzania katika michuano hiyo ni ABC iliyopoteza dhidi ya Remesha ya Burundi kwa pointi 84-75.

Related Articles

Back to top button