Chidumule alia na ‘sapoti’ muziki wa injili

DAR ES SALAAM: MSANII wa Muziki wa Injili nchini Cosmas Chidumule amewataka watangazaji wa wamiliki wa vyombo vya habari kuacha kutoza pesa ili kupiga nyimbo za waimbaji wa nyimbo za dini.
Akizungumza na Spoti Leo Chidumule amesema ili kukuza na kuzidi kuinua wasanii wachanga wa nyimbo za Injili watangazaji wa vipindi hivyo wanapaswa kutoa sapoti.
“Muziki wa Injili unawategemea kwa asilimia kubwa watangazaji kupiga kazi zao ili kuzidi kuutangaza na kuinua muziki huo inapaswa kuwapa ushirikiano hata wanapokuwa hawana kitu.
“Kwa sababu nyimbo za Injili zinaponya watu wanaposikiliza na kuwasaidia mashabiki kumjua Mungu Kupitia nyimbo za Injili hivyo wanapaswa kusapotiwa kwa kiasi kikubwa.”amesema Chidumule
Pia ameongeza kuwa wakisapoti waimbaji hao itakuwa sehemu moja wapo ya kutangaza Injili wakati kwa kutumia vipawa vyao.