Nyumbani

CHAN ni sehemu ya maandalizi ya fainali za AFCON

DAR ES SALAAM: MWENYEKITI wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Leodegar Tenga amesema  mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) ni sehemu ya maandalizi ya AFCON ya 2027.

Tenga ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ya CHAN na AFCON , amesema mashindano ya CHAN yanatarajia kuanza Februari 1 hadi 28, Tanzania wenyeji wa mashindano hayo.

“Ombi kubwa kwa Shirikisho la mpira wa miguu Afrika (CAF) kutaka uwenyeji wa AFCON lakini tumepewa kuandaa CHAN ikiwa sehemu ya maandalizi ya mashindano hayo ya 2027 ambayo yatafanyika Tanzania, Kenya na Uganda.”

“Watanzania wajitayarishe kwa fursa, kwa sababu tunataraji kupokea wageni kutoka mataifa mbalimbali, ambao wataongeza uchumi wa Taifa kwa kutembelea katika sehemu zetu za vivutio,” amesema.

Tenga pia amesema mashabiki kujitokeza kwa wingi katika mashindano hayo ambayo inatoa taswira ya jinsi gani AFCON itakavyokuwa.

Amesema  timu zinazoshiriki zinaanza kuwasili   nchini Januari 24, viwanja viwili Benjamin Mkapa na  New Amaan Complex, Visiwani Zanzibar kutumia katika mashindano hayo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button