EPL

Carrick kuibeba United hadi mwisho wa msimu

MANCHESTER:MANCHESTER United wamethibitisha rasmi kumteua Michael Carrick kuwa kocha wa muda wa kikosi cha kwanza hadi msimu utakapomalizika. Carrick anachukua nafasi hiyo baada ya Darren Fletcher aliyekuwa anakaimu kwa muda mfupi kufuatia kufutwa kazi kwa Ruben Amorim wiki iliyopita.

Carrick, ambaye pia alikuwa akiwania nafasi hiyo na Ole Gunnar Solskjaer, amechaguliwa kutokana na uzoefu wake mkubwa ndani ya klabu. Atakiongoza kikosi hicho kuanzia dabi kali ya Manchester dhidi ya City Jumamosi hii katika dimba la Old Trafford.

Mchezaji huyo wa zamani wa kiungo ameichezea Manchester United kwa miaka 12, akitwaa mataji 18 makubwa ikiwemo ubingwa wa Ligi Kuu England mara tano na Ligi ya Mabingwa Ulaya ya mwaka 2008. Uzoefu huo wa ndani unatajwa kuwa sababu kubwa ya kuaminiwa kwake katika kipindi hiki cha mpito.

Carrick mwenye umri wa miaka 44 anarejea Old Trafford baada ya kipindi cha miaka mitatu akiwa kocha wa Middlesbrough kwenye Championship. Msimu uliopita aliiongoza timu hiyo kumaliza nafasi ya 10, wakikusanya pointi 64 katika mechi 46.

United wanaamini kuwa uelewa wa Carrick kuhusu klabu, pamoja na uongozi wake tulivu, vinaweza kusaidia kuleta utulivu ndani ya kikosi ambacho kimekuwa kikiyumba msimu hu

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button