Burna Boy kutumbuiza Nairobi,Kenya Machi 1,2025

BINGWA wa tuzo za Grammy, Burna Boy anatazamiwa kuwa miongoni mwa watumbuizaji katika tamasha la ‘MadfunXperience’ linalotarajiwa, kufanyika Uhuru Gardens jijini Nairobi mnamo Machi 1, 2025.
Tamasha hilo liimeandaliwa na Kampuni ya utengenezaji matukio, usafiri na tiketi ya Madfun, huku ikiahidi kufanya tamasha la kihistoria la burudani nchini Kenya kwa mwaka huu.
Watakaojiunga na Burna Boy kwenye tamasha hilo ni mwimbaji wa Afro-pop wa Kenya, Charisma na mwimbaji maarufu wa Amapiano Virgo Deep kutoka Afrika Kusini, pamoja na ma-DJ mashuhuri.
Mkurugenzi Mkuu wa Madfun, Joy Wachira, amesema lengo la tamasha hilo ni kuinua sanaa na burudani ya kimataifa kwa wasanii wa Kenya.
“Ni wakati wa kuinua kiwango na kuunda utamaduni wa muziki wa Afrika. Tuko hapa kuthibitisha kwamba Kenya ina uwezo wa kuandaa hafla za kimataifa zinazoshindana na walio bora zaidi duniani. MadfunXperience ni zaidi ya tamasha kupitia hili tamasha tunataka kuonyesha nafasi ya Kenya katika tasnia ya burudani kimataifa.”
Mara ya mwisho mwimbaji huyo kutoka Nigeria alitumbuiza nchini Kenya mwaka wa 2019.