Masumbwi

Bondia aliyefariki kwa TKO kuzikwa mwaka mpya

SIKUya mazishi ya bondia Hassan Mgaya imesogezwa mbele ambapo hatozikwa siku ya leo Desemba 30, 2024 bali atazikwa jumatano ya Januari Mosi mwaka 2025.
Taarifa hiyo iliyotolewa na mweka hazina wa chama cha mabondia nchini Tanzania, Cosmas Cheka, imekuja baada ya baba yake kuomba mwanae asizikwe hadi atakaporudi kutoka nchini Congo ili aweze kumzika mtoto wake.
“Wadau wa ngumi, napenda kutoa taarifa ya mazishi ya bondia Hassan Mgaya kilichotokea jana hospitali ya Mwananyamala, mazishi yake yatafanyika jumatano ya siku ya mwaka mpya. Mzee wake ameomba mpaka yeye atakaporudi kutoka DR Congo,” ilisema taarifa hiyo ya Cheka.
Mgaya alipoteza maisha siku ya jumapili Desemba 29 mwaka huu katika hospitali ya Mwananyamala kufuatia kupigwa kwa TKO na mpinzani wake Paulo Elias katika pambano lake lililofanyika usiku wa Desemba 29, 2024 kwenye ukumbi wa Dunia ndogo uliopo Tandale kwa mtogole.

Related Articles

Back to top button