Bondia akimbia na mkanda baada ya Rehema kushinda

ZANZIBAR: KOCHA wa bondia wa ngumi za kulipwa kutoka nchini Uingereza mwenye asili ya India, Prince Patel amewafanyia fujo kamisheni ya Ngumi za kulipwa Zanzibar (ZaPBC) usiku wa kuamkia jana kwa sababu ya bondia wake Sangeeta Birdi.
–
Inaelezwa kuwa kocha huyo usiku wa kuamkia leo amewafanyia fujo katibu wa kamishi ya ngumi za kulipwa Zanzibar, Nasibu Amour na kocha Sharif Muhsin kufuatia Patel kugoma kuachia mkanda wa ubingwa wa PST, baada ya bondia wake Sangeeta Bird kupigwa kwa pointi jana visiwani humo dhidi ya Rehema Abdallah mtanzania.
–
Katibu wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Zanzibar, ZaPBC, Amour ameeleza fujo hizo zilifanyika katika pambano hilo jana kwenye ukumbi wa Magereza na kupelekea kutokea na mzozo mkubwa uliomalizwa leo na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa visiwani.
–
“Makubaliano yalikuwa ni kucheza Ubingwa wa Pugilistic Syndicate of Tanzania (PST ) dhidi ya Sangeeta, Muingereza mwenye asili ya India aliyezaliwa nchini Canada kwenye pambano hilo la raundi 10.Katika pambano hilo, Rehema alishinda, sababu ya bondia huyo wa kigeni kutokubali kuachia mkanda na kukimbia nao hadi hoteli aliyofikia na tulipokwenda kuchukuwa mkanda akaazisha fujo na kukimbilia ndani kwa kuhofia na kuchukua kitu cha hatari na kuja kutudhuru,” amesema Amour.
–
Ameeleza kuwa uongozi wa Kamisheni umehakikisha wanamaliza suala hilo kwa bondia Rehema kupata haki ya ushindi wake aliupata katika pambano hilo na alipoulizwa juu ya suala la kufanyiwa vurugu kiongozi huyo alisisitiza tayari suala hilo wameshalimaliza na kila mmoja anaendelea na mambo yake.