Ligi KuuNyumbani

Bocco amtabiria Mayele ufungaji bora

NAHODHA wa timu ya Simba, John Bocco amesema mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele ana nafasi kubwa ya kubeba tuzo ya mfungaji bora msimu huu.

Akizungumza na SpotiLeo Bocco amesema hiyo inatokana na mshambuliaji huyo kuwa katika kiwango bora hivi sasa ukilinganisha na washambuliaji wengine.

Nahodha wa Simba, John Bocco.

“Niseme ukweli Mayele ana nafasi kubwa ya kuwa mfungaji bora msimu huu kutokana na rekodi zake na idadi ya mabao aliyofunga hadi sasa,” amesema Bocco.

Nahodha huyo wa Simba amesema mshambuliaji mwenzake wa Simba, Moses Phiri alianza vizuri lakini majeraha aliyoyapata na tofauti aliyopitwa na Mayele inaweza kuwa ngumu kumfikia.

Mpaka sasa Mayele amefunga mabao 14 kwenye ligi kuu msimu huu huku anayemfuatia Phiri wa Simba akiwa na mabao 10, timu zote zikibakisha michezo 12 kabla msimu kumalizika.

Related Articles

Back to top button