Nyumbani

Et kuna watu wameiga Simba Day?

Heee!! Mmesikia huko? Et kuna timu imeiga tamasha la Simba Day? Mbona Mwenyekiti wa Simba Murtaza Mangungu amesema kuwa watu wameiga kwao wakatoa neno ‘Day’ wakaweka ‘Wiki’.

Sawa hebu tuchambue hapa! Ukiachana na Simba SC, timu zinazofanya matamasha ya aina hii ni Yanga SC na Singida Fountain Gate, la Singida linatiwa ‘Singida Big Day’ neno ‘Day’ halijaondolewa hapo, tamasha la Yanga linaitwa Wiki ya Wananchi sasa ni wazi kuwa Mangungu ameikusudia Yanga kuwa ndio wameiga maana ndio wanaotumia neno ‘Wiki’

Lakini wanasemaga kitu kizuri kinaigwa, kuna shida kwani Yanga kuiga kizuri kutoka kwa watani wao? Kwani sio hawa wakikaa vijiweni wanasema ni wa baba mmoja na wengine wanasema mmoja katokea ubavuni kwa mwenzie.

Labda pengine tabu ya hizi timu mbili huwa hazitaki kuonekana mmoja yuko chini ya mwenzie au hawapendi kujishusha na shida huanzia hapo, sawa basi tuiache kama ilivyo.
Niambie wewe ni kweli Yanga imeiga kutoka kwa Simba?

Related Articles

Back to top button