
NIGERIA: FURAHA inaongezeka nchini kote Big Brother Naija inaporejea wikendi hii kwa msimu wake wa 10 wa kihistoria.
Onesho hilo linaanza leo kwa onesho la mara mbili Jumamosi, Julai 26 (leo) na Jumapili, Julai 27 (kesho), toleo la mwaka litakuwa na mchezo wa kuigiza na matukio ya kiburudani zaidi kuliko hapo awali na zawadi kuu itakuwa ₦ milioni 150, ndiyo itakayotolewa kwa mshinid ambayo ni kubwa zaidia ya zawadi iliyokuwa ikitolewa awali.
Mtangazaji Ebuka Obi-Uchendu atawakaribisha wa nyumbani ambao wanatarajiwa kuwa kivutio kwa watazamaji kwa muda wa wiki 10, huku fainali ya onesho hilo ikitarajiwa kuwa Oktoba 5.
Tangu ilipoanza mwaka 2006, BBNaija imetoa tuzo za ₦ milioni 637. Mshindi wa msimu uliopita, Kellyrae, aliweka historia kuwa mshirika wa kwanza mama wa nyumbani kushinda tuzo na pesa za Naigeria Naila 100 milioni.
Maonesho hayo yatakuwa yakionekana kuanzia saa 7 p.m. kwenye chanel ya Africa Magic Showcase, Familia, na Showmax. Pia itarushwa moja kwa moja kwa saa 24 kupitia DStv Channel 198, GOtv Channel 49, na nyingine nyingi