Bei ya Bellingham bil 348/-

MANCHESTER United, Chelsea na Liverpool zitalazimika kuongeza zaidi dau tofauti na ombi lao la pauni milioni 87 sawa na shilingi bilioni 233.2 lilizopanga kumsajili kiungo wa Borussia Dortmund ya Ujerumani, Jude Bellingham.
Ripoti kutoka Ujerumani zimesema miamba hiyo ya Bundesliga inataka pauni zinazofikia milioni 130 sawa na shilingi bilioni 348.5 ili kumuuza nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 19 huku mabingwa wa La Liga, Real Madrid pia ikimtolewa macho.
Inasemekana Chelsea inaongoza mbio za kumsajili Bellingham ili kupata kipaji kipya na chipukizi ambaye Kocha Graham Potter anaweza kufanya kazi naye baada ya kuchukua mikoba ya Thomas Tuchel.
Dortmund imefanikiwa kuwauza wachezaji wake bora vijana kwa kiasi kikubwa cha fedha katika miaka michache iliyopita na inaonekana itafanya hivyo kwa Bellingham.