Kwingineko

Pigo zito Netherlands

Timu ya Taifa ya Uholanzi imepata pigo siku chache kabla ya kuanza kwa michuano ya Euro 2024.

Hii ni baada ya kuthibitisha kwamba mmoja kati ya wachezaji muhimu wa timu hiyo na wa kutegemewa kushindwa kupona majeraha yaliyokuwa yakimkabili kwa wakati,na sasa atayakosa mashindano hayo yote.

Mchezaji huyo si mwingine bali ni Staa wa Barcelona, Frenkie De Jong ambaye alipata majeraha ya kifundo cha mguu dhidi katika mechi dhidi ya Real Madrid mwezi Aprili.

Licha ya majeraha hayo, De Jong,27, aliwekwa katika orodha ya mwisho ya wachezaji 26 kwani kocha Ronald Koeman alikuwa na imani kwamba kiungo huyo angerejea angalau katika michezo ya mwisho ya makundi.

Lakini kupitia ukurasa wake wa Instagram, De Jong ameandika “Nina huzuni na masikitiko kwamba sitaweza kucheza katika michuano ya Ulaya.Tumefanya kazi kubwa wiki chache zilizopita lakini isivyo bahati kifundo changu cha mguu kinahitaji muda zaidi kupona”.

Wakiwa wamepangwa katika kundi E, Uholanzi itaanza kampeni yake ya michuano hii siku ya jumapili ambapo itamenyana na Poland pale Volksparkstadion.Kisha watamenyana na Ufaransa tarehe 21 Juni kisha kumalizia na Ausrtia wiki moja baadae.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button