AY na wasanii wamuenzi Rais Samia

DAR ES SALAAM: AMBWENE Yesaya, msanii mkongwe wa bongo fleva kwa kushirikiana na wasanii wenzake wameachia wimbo maalumu uitwao “Twende Nae Sawa”, kumsapoti Rais Samia Suluhu kuelekea kwenye uchaguz mkuu.
Nyota huyo ametambulisha wimbo huo leo na kuandika ujumbe kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii, akisema umetolewa kwa heshima ya Rais, Dk Samia Suluhu Hassan, pamoja na Chama cha Mapinduzi (CCM) na Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM).
Katika ujumbe wake, AY aliwashukuru wasanii walioshirikiana naye kwenye mradi huo akiwemo Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma ‘Mwana Fa’, Chege Chigunda, Hamad Seneda ‘Madee’, Joel Lwaga, Mzee Yussuf, Nicolas Lyimo ‘Billnass’, Dulla Makabila, Kheri Sameer ‘Mr Blue’, na The Hanstone Nation.
Wimbo huo unatarajiwa kuwa sehemu ya hamasa za kisiasa na kijamii kuelekea uchaguzi mkuu ujao, ambapo muziki umetumika kama daraja la kuunganisha vijana na wananchi.