Arsenal kukutana na Leverkusen hatua ya 16

NYON:ARSENAL wamepangwa kukutana na Bayer Leverkusen katika hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya 2025/26, droo ambayo tayari imeanza kuvuta hisia kutokana na stori inayomuhusu Kai Havertz.
Havertz, ambaye ni zao la akademi ya Leverkusen, alipandishwa kikosi cha kwanza mwaka 2016 kabla ya kuhamia Chelsea majira ya kiangazi 2020. Mwaka 2023 akasajiliwa na Arsenal. Sasa anaenda kukutana na klabu iliyomlea kwenye hatua ya mtoano ya Ulaya.
Kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya,Wamekutana mara kwenye mechi 2 tu za msimu wa 2001/02. Leverkusen walitoa sare ya 1-1 nyumbani kabla ya kushinda 4-1 ugenini dhidi ya Arsenal. Msimu huo Arsenal walimaliza wa tatu kwenye kundi lao wakiwa na pointi saba na wakaondolewa, wakati Leverkusen waliongoza kundi kwa pointi 10 na baadaye wakafika hadi fainali ya mashindano ambapo walifungwa 1-2 na Real Madrid.
Safari hii, nani atasonga mbele?




