Africa

Arajiga ni mmoja tu

BERKANE: Historia inaenda kuandikwa leo, Waamuzi Watanzania kuchezesha mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC), RS Berkane ya Morocco dhidi ya Stellenbosch kutoka Afrika Kusini.

Ahmed Arajiga atakuwa Mwamuzi Mkuu ‘pilato’ wa mchezo wa leo unaopigwa Manispaa ya Berkane nchini Morocco ikiwa ni hatua muhimu kwa waamuzi wa Kitanzania kupata fursa kama hii katika mashindano ya kimataifa.

Mwamuzi mwengine ni Nasir Salum Siyah maarufu Msomali kutoka Zanzibar.

Hii ni heshima kubwa kwa Tanzania pia, ni ushahidi wa maendeleo ya soka la Tanzania si tu kwa wachezaji, bali pia kwa waamuzi ambao wanajitokeza katika viwango vya juu barani Afrika.

Mchezo huu wa CAFCC unatarajiwa kuwa na ushindani mkali, na uteuzi wa Arajiga na timu yake ya waamuzi unadhihirisha imani ya CAF katika uwezo wao wa kusimamia mechi kubwa.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button