EPLKwingineko
Anthony amwaga wino Man United kwa bil 220.9/-

KLABU ya Manchester United imekamilisha kumsajili winga wa Brazil, Antony Matheus dos Santos ‘Anthony’ kutoka Ajax ya Uholanzi kwa ada ya awali ya pauni milioni 82 sawa na shilingi bilioni 220.9.
Usajili huo unaojumuisha nyongeza ya pauni milioni 4.3 sawa na shilingi ni wa nne ghali zaidi katika historia ya Ligi Kuu Uingereza.
Anthony mwenye umri wa miaka 22 ametia saini mkataba hadi 2027 wenye chaguo la kuongoza mwaka mmoja.
Usajili mwingine uliovunja rekodi ni wa Jack Grealish kutoka Aston Villa kwenda Manchster City kwa pauni milioni 105.75, Romelu Lukaku kutoka Inter Milan kwenda Chelsea kwa pauni milioni 101.70 na Paul Pogba kutoka Juventus kwenda Man United kwa pauni milioni 94.50.