KwinginekoLa Liga

Real kumsajili Bellingham kwa zaidi ya bil 248/-

KLABU ya Real Madrid imeripotiwa kukubaliana na Borussia Dortmund ada ya zaidi ya pauni milioni 86 sawa na shilingi bilioni 248.7 ili kumsajili kiungo Jude Bellingham, mtandao wa michezo wa The Athletic umeripoti.

Kwa kiasi kikubwa nyota huyo wa kimataifa wa England amekuwa akitarajiwa kujiunga na Real Madrid.

Bellingham ndiye anayewaniwa zaidi majira haya ya joto baada ya kiwango chake bora katika timu ya Dortmund na England huku vilabu kadhaa vikubwa Ulaya vikiwemo Manchester City, Chelsea na PSG vikionesha nia.

Ushindani wa karibu zaidi ambao Real ilikabiliana nao ulitoka kwa City, lakini miamba hiyo ya Hispania imeibwaga timu hiyo ya Kocha Pep Guardiola baada ya kumpa kandarasi ya miaka sita.

Bellingham alihamia Ujerumani akitokea Birmingham mwaka 2020 akiwa na umri wa miaka 16 na tayari familia yake imeanza kutafuta makazi katika jiji la Madrid.

Related Articles

Back to top button