Kwingineko

Alonso:Kombe lile halikuwa na umuhimu mkubwa kwetu

JEDDAH:BAADA ya kupoteza fainali ya Super Cup dhidi ya Barcelona, kocha Xabi Alonso amesema wazi kuwa kwa mtazamo wake, hilo lilikuwa shindano lisilo na uzito mkubwa ukilinganisha na mengine wanayoshiriki msimu huu.
Akizungumza baada ya mechi hiyo ngumu na yenye ushindani mkubwa, Alonso ameonesha kutokukatishwa tamaa na matokeo, akisisitiza kuwa timu yake inapaswa kufunga ukurasa haraka na kuelekeza nguvu kwenye malengo makubwa zaidi yanayowasubiri.
“Ninapaswa kuwapongeza Barcelona. Ilikuwa mechi ngumu sana kuanzia mwanzo hadi mwisho. Tulicheza dhidi ya timu bora na mchezo ulikuwa wa ushindani mkubwa. Mwishoni tulipata nafasi mbili nzuri za kusawazisha, lakini hatukuweza kuzitumia,” alisema Alonso.
Kocha huyo amesema kupoteza fainali hiyo hakubadilishi mwelekeo wa msimu wao, akieleza kuwa bado wana mashindano muhimu zaidi ya kupigania, na ndio maana hataki kuona wachezaji wake wakikaa kwenye majonzi kwa muda mrefu.
“Kupoteza fainali? Kwa uhalisia, hili ndilo shindano lenye umuhimu mdogo zaidi kwetu msimu huu. Ndiyo maana tunapaswa kufunga ukurasa haraka iwezekanavyo na kuelekeza mawazo yetu kwenye mashindano mengine ambayo ni muhimu zaidi,” ameongeza.
Alonso pia ameonesha jinsi alivyoamini timu yake hata baada ya kuruhusu bao la tatu, akisema bado alikuwa na uhakika wa kupata nafasi za kurudi mchezoni, jambo ambalo kwa kiasi kikubwa lilitokea, japokuwa walishindwa kulimalizia.
 
“Walipofunga bao la tatu, nilikuwa na uhakika wa asilimia mia moja kwamba tutapata nafasi za kusawazisha. Na tulizipata. Lakini mpira tu haukuingia. Timu imeonesha moyo mkubwa, kujituma na nidhamu, lakini tulikosa ule umakini wa mwisho ambao ungeweza kutupeleka mpaka penalti,” alisema.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button