Habari Mpya

Lewandowski gumzo Bayern ikiikabili Barca

KATIKA usiku wa Ulaya leo michezo 7 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya inapigwa huku mchezo mkubwa zaidi ukiwa Bayern Munich kuikaribisha Barcelona na mshambuliaji wa zamani Robert Lewandowski kwenye uwanja wa Allianz Arena.

Mshambuliaji huyo wa Poland alihama kutoka Bavaria kwenda Catalunya msimu huu baada ya kucheza miaka 8 Ujeurumani akifunga mabao 344 na akiwa amejithibitishia kuwa mkongwe wa muda wote klabu hiyo ya Bavaria.

Mwishoni mwa msimu uliopita Lewandowski mwenye umri wa miaka 34 alitangaza kuwa “muda wake Munich umefikia mwisho” na alihamia Barca kwa karibu pauni milioni 42.5 sawa na shilingi bilioni 115.1.

Ratiba ya michezo mingine ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ni kama ifuatavyo:

Liverpool                 vs      Ajax
Bayer Leverkusen    vs      Atletico Madrid
FC Porto                  vs     Club Brugge
Viktoria Plzen           vs     Inter Milan
Sporting CP             vs      Tottenham Hotspur
Marseille                  vs       Eintracht Frankfurt

Related Articles

Back to top button