Africa

JKT Queens kuwania tuzo CAF

KLABU ya mpira wa miguu ya wanawake JKT Queens imechaguliwa kuwania tuzo ya kipengele cha klabu bora ya mwaka kwa wanawake ya Shirikisho la Mpira wa Mguu Afrika(CAF).

Kwa mujibu wa CAF, Winfrida Gerald wa JKT Queens mwenye umri wa miaka 15 amechaguliwa kushindania tuzo ya mchezaji bora chipukizi wakati Najiat Abass atawania tuzo ya kipa bora.

Kocha wa JKT Queens, Ester Chabruma amechaguliwa kuwania kipengele cha kocha bora.

Pia timu ya taifa ya wanawake imechaguliwa kuwania tuzo ya timu bora ya taifa ya wanawake.

Sherehe za utoaji tuzo za CAF zitafanyika katika jiji la Marrakech, Morocco Desemba 11, 2023.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button