Tetesi

Tetesi za usajili Ulaya

KLABU ya Manchester United itajaribu kuwania saini ya winga wa Bayern Munich, Serge Gnabry wakati wa dirisha la uhamisho Januari, 2024 huku kocha wa mashetani hao wekundu Erik ten Hag akiwa na nia ya kumsajili fowadi huyo mahiri. Real Madrid pia inamtupia jicho mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani. (El Nacional)

Mshambuliaji wa RB Leipzig, Benjamin Sesko amekiri alikataa uhamisho kwenda Manchester United akisisitiza alifanya chaguo sahihi kwenda Bundesliga badala yake.(Transfermarkt)

Barcelona imefikia makubalioano kwa maneno na Manchester City kuhusu ada ya uhamisho pauni milioni 30.4 ya Joao Cancelo, ambaye kwa sasa upo kwa mkopo La Blaugrana.(El Chiringuito)

Mlengwa wa ghafla wa usajili Barcelona ni Wilfred Ndidi, ambaye mkataba wake Leicester City unamalizika majira yajayo ya kiangazi. Ndidi alishindwa kuondoka King Power Stadium kufuatia Leicester kushuka daraja kwenda Championship.(SPORT)

Wakala wa mshambuliaji wa Aston Villa, Ollie Watkins amefanya mazungumzo na mkurugenzi wa michezo wa Arsenal Edu kuhusu uwezekano wa uhamisho. Pia Chelsea inavutiwa na mchezaji huyo wa kimataifa wa England.(Football Transfers)

Mshambuliaji mahiri wa Brentford ‘The Bees’, Ivan Toney bado yupo katika orodha za wachezaji wanaohitajika kusajiliwa Arsenal na Chelsea, ingawa The Bees inaonekana itang’ang’ania ada ya pauni milioni 80.(ESPN)

Rais wa Laliga Javier Tebas anaamini Kylian Mbappe atahamia Hispania majira yajayo ya kiangazi, huku Real Madrid ikionekana ndio itakayomsajili fowadi huyo kwa uhamisho huru toka PSG.(Movistar+)

Liverpool itahitaji huduma ya fowadi wa Juventus Federico Chiesa iwapo majogoo hao wa Liverpool watachagua kumuuza Mohamed Salah majira yajayo ya kiangazi.(Fichajes)

Chiesa atakuwa tayari kujiunga na Liverpool iwapo nafasi itapatikana.(Corriere dello Sport)

Juventus inaweza kumpa ofa Pierre-Emile Hojbjerg kuondoka Tottenham wakati wa dirisha la uhamisho Januari, 2024. Mchezaji huyo wa Denmark amepoteza nafasi yake kwa Yves Bissouma katika kikosi cha kocha Ange Postecoglou.(Corriere della Sera)

Related Articles

Back to top button