Tetesi

Folarin Balogun akaribia kukiwasha Monaco

MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Folarin Balogun anakaribia kuhamia Monaco kwa ada ya pauni milioni 35 sawa na shilingi bilioni 107.5 licha ya kuwaniwa na Chelsea na Inter Milan.

Ripoti zimesema majadiliano yanaendelea lakini Balogun mwenye umri wa miaka 22 anatarajiwa kurejea Ufaransa ambako aliitumikia Reims kwa mkopo msimu uliopita akifunga mabao 22.

Balogun aliyezaliwa New York, Marekani alihamia London akiwa mtoto na kukulia kwenye mfumo wa kukuza vipaji vya soka wa Arsenal.

Related Articles

Back to top button