Tetesi

Tetesi za Usajili

MANCHESTER United imetoa ofa rasmi ya mkopo kwa beki wa kushoto wa Chelsea, Marc Cucurella na klabu hizo mbili ziko kwenye mazungumzo kuhusu uwezekano wa kumnunua.(The Athletic)

Wakati Luke Shaw na Tyrell Malacia wakiwa majeruhi, Manchester United inaangalia machaguo kadhaa ya mabeki, akiwemo Nicolas Tagliafico wa Lyon, ambaye awali alikuwa chini ya kocha Erik ten Hag katika klabu ya Ajax. (Le Parisien)

Barcelona inaandaa mpango maalum wa kumsajili Joao Felix ndani ya miongozo ya haki ya kifedha ya uchezaji kabla ya kumalizika kwa dirisha la usajili. Mshambuliaji huyo wa Atletico Madrid anapendelezea kuhamia Katalunya na atafikiria tu timu nyingine iwapo uhamisho huo utakwama. (Fabrizio Romano)

Liverpool inaangalia iwapo ina fedha za kusajili kiungo zaidi ya mmoja kabla ya tarehe ya mwisho ya dirisha la usajili na uhamisho. Cheick Doucoure wa Crystal Palace ni ghali zaidi, huku Wilfred Ndidi wa Leicester akizingatiwa. (Independent)

Arsenal inasisitiza kwamba Emile Smith Rowe hatauzwa majira haya ya joto kufuatia nia ya wapinzani wake wa London, Chelsea kutaka kumsajili.(Evening Standard)

Related Articles

Back to top button