
UPEPO wa ‘Thank You’ unaendelea kuvuma katika klabu mbalimbali, safari hii ukimpuliza Erasto Nyoni wa Simba.
Saa chache zilizopita wekundu hao wa Msimbazi walitangaza kuachana na golikipa Beno Kakolanya baada ya mkataba wake kumalizika.
Katika taarifa yake Simba imesema :”Uongozi wa klabu unautangazia umma kuwa hatutaendelea kuwa na mchezaji wetu kiraka Erasto Nyoni baada ya mkataba wake kumalizika,”imesema Simba.
Kabla ya Thank You za leo Simba tayari ilikwisha tangaza kuachana na Mohamed Ouattara, Nelson Esor-Bulunwo Okwa na Victor Akpan.