Ligi Kuu

Simba yatemana na Akpam

KATIKA mwendelezo wa kupunguza baadhi ya wachezaji na kuongeza wengine kwa ajili ya msimu ujao, Simba SC imeagana na kiungo Victor Akpam.

Klabu hiyo yenye maskani yake Msimbazi imetoa taarifa ya kuachana na mchezaji huyo kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii.

“Baada ya kuwa kwenye kikosi chetu kwa msimu mmoja, Victor Akpan hatakuwa sehemu ya timu yetu ya msimu ujao.” Imeeleza taarifa hiyo.

Simba ilimsajili Akpam akitokea Coast Union ya Tanga na sasa Mnaigeria huyo yuko huru.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button