Tetesi

Bayern yahamia kwa Rice

KWA mujibu wa mtandao wa Sky Sport nchini Ujerumani, Bayern Munchen wanaangalia uwezekano wa kuinasa asaini ya kiungo, Decline Rice kutoka West Ham United.

Nyota huyo raia wa Uingereza anawindwa pia na klabu ya Arsenal ambayo inataka kumsajili kama mbadala wa Granit Xhaka ambaye anatimkia Bayer Leverkusen, kwa mujibu wa mwandishi wa zamani wa Sky Sport, Fabrizio Romano.

Rice ,24, mkataba wake na West Ham unaisha 2024, hivyo timu hiyo haipo tayari kumuacha aondoke bure mara baada ya mkataba wake kuisha.

Uwezekano wa kiungo huyo kusalia klabuni hapo ni mdogo kutokana na baadhi ya timu kubwa kutaka huduma yake licha ya dau kubwa la pauni milioni 100 lililowekwa na West Ham.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button