Wachezaji wa kikosi cha Al Ahly ya Misri wakifanya mazoezi kueleka mchezo dhidi ya Al Hilal.
BAADA ya wekundu wa Msimbazi, Simba kupokea kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa Raja Casablanca ya Morocco katika mchezo wake wa mwisho Ligi ya Mabingwa Afrika kundi C, michuano hiyo inaendelea leo kwa mechi tatu.
Patashika kubwa itakuwa kundi B wakati Al Ahly ya Misri itakuwa nyumbani kuikaribisha Al Hilal ya Sudan huku Ahly ikihitaji ushindi na Al Hilal ikihitaji sare ili kuingia robo fainali.
Katika mchezo mwingine wa kundi hilo Coton Sport ni mgeni wa Mamelodi Sundowns iliyokwisha kata tiketi ya robo fainali.
Nayo Petro Atletico ya Angola itakuwa uwanja wa nyumbani kuikaribisha AS Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo katika mchezo wa kundi A.