Africa

Simba, Yanga kishindo CAF

KILA kona linapozungumziwa soka kwa sasa, mashabiki wa Simba na Yanga hawachekani
bali wanapongezana, wakati mwingine wanatamba kuwa kila mmoja ataendelea kufanya vizuri kwenye michuano ya klabu Afrika.

Hiyo imetokana na moto uliowashwa na timu hizo kwenye hatua za makundi za michuano
hiyo na sasa wamedondokea kwenye robo fainali. Ndio timu pekee zilizosalia kwenye michuano hiyo baada ya safari ndefu ya uwakilishi wa timu sita kutoka Tanzania Bara na Visiwani.

KMKM na Kipanga za Zanzibar zilitupwa nje kwenye hatua ya awali ya kuwania kuingia
makundi ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika. KMKM ilichapwa jumla ya  mabao 6-0 kutoka kwa Al Ahly Tripoli ya Sudan.

Kipanga ikabugizwa mabao 7-0 na Club African ya Tunisia. Azam na Geita Gold zilikwama pia katika hatua hiyo. Geita ilitolewa kwa faida ya bao la ugenini na Hilal Alsahil ya Sudan baada ya kufungwa bao 1-0 ugenini kisha kupata ushindi wa mabao 2-1 nyumbani.

Azam ilifungwa mabao 3-0 ugenini na Al Akhdar ya Libya kabla ya ushindi wa mabao 2-0 nyumbani. Hata hivyo, Yanga nayo iliyumba kufuzu kuingia makundi ya Ligi ya Mabingwa, ikadondokea makundi ya Kombe la Shirikisho na hivyo kupata wawakilishi wawili kwenye michuano miwili mikubwa Afrika.

ZAANZA VIBAYA
Simba kwenye Ligi ya Mabingwa ilianza vibaya makundi kwa kufungwa bao 1-0 ugenini na Horoya AC kabla ya kuruhusu kufungwa mabao 3-0 na Raja Casablanca, Uwanja wa
Mkapa, Dar es Salaam.

Ni kama vile ilivyoanza Yanga kwa kufungwa mabao 2-0 na US Monastir ugenini. Hata hivyo, timu hizo zikaibuka na kuanza kuzoa pointi mfululizo, Simba ikaamka na kuibutua Vipers nyumbani na ugenini kwa ushindi wa bao 1-0 kabla ya kuididimiza Horoya Uwanja
wa Mkapa kwa mabao 7-0.

Yanga nayo ikarejea kwa Mkapa na kuichapa TP Mazembe mabao 3-1, kisha ikatoa sare na kuifunga Real Bamako kabla ya kulipa kisasi cha mabao 2-0 kwa US Monastir ya Tunisia.
Kwa matokeo hayo na ushindi mkubwa wa Simba hatua ya makundi msimu huu, ukaifanya kutimiza alama tisa nyuma ya 13 za Raja na kutinga robo fainali.

Ni kama vile Yanga ilivyowachapa Waarabu na kuongoza Kundi D kwa alama 10 sawa na Monastir, lakini Yanga ikiwa na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga. Lazima mashabiki watambe, kutoka kufanya vibaya mpaka kutinga robo timu zikiwa na mchezo mmoja
mmoja mkononi.

BAO LA MAMA
Hata hivyo, timu hizo zilifanya vizuri pia kwa kile kilichoonekana ni chagizo la hamasa kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye baada ya timu hizo kupoteza mechi za kwanza, akaweka ahadi ya kutoa Sh milioni 5 kwa kila bao litakalofungwa na timu hizo.

Morali hiyo ambayo haijawahi kuwekwa tangu kuanzishwa kwa Tanzania, ilitendewa haki na wachezaji wa timu hizo kwani kila linapofungwa bao mashabiki wanahesabu fedha wanazoingiza na mwisho kujikuta wamefaulu kuingia hatua inayofuata.

AFRIKA MASHARIKI
Mbali na ahadi hiyo kuwekwa kwa mara ya kwanza, lakini pia imekuwa mara ya kwanza kwa timu hizi mbili kusonga robo fainali za michuano Licha kwa rekodi ndio timu kutoka kwenye kwa uwezo Afrika imewakilishwa vyema.

Pia ni kwa Afrika kuonekana kusikika kona ya Afrika kama vile ambavyo wachezaji wa Simba na Yanga wanavyopishana kwenye vikosi vya wiki vya michuano hiyo kila baada ya kumalizika kwa mechi.

Inadhihirisha kuwa Tanzania haikubahatisha kuingia kwenye tano bora ya ligi zenye ushindani Afrika na pia ni ligi pendwa Afrika Mashariki na Kati kutokana na udhamini mkubwa wa matangazo na ufuatiliaji wa mashabiki wake.

Baada ya muda mrefu, soka la Afrika kwa ngazi ya klabu kutawaliwa na klabu za Kaskazini, Afrika Magharibi, angalau Afrika ya Kusini, sasa ni zamu pia ya Afrika Mashariki kupitia
Simba na Yanga.

Vilevile, kulingana na pointi zinazowekwa na Caf kwa nchi husika kuingiza timu nne kwenye
michuano hiyo msimu ujao, Tanzania imezidi kujiongezea pointi zinazowatoa nafasi ya 11 ya uwakilishi na kuingia kwenye 10 bora.Pointi hizo huongezwa kwa usahihi baada ya kumalizika kwa michuano.

VINARA WA MABAO
Kama haitoshi timu hizi kufanya vyema lakini pia wachezaji bin- fasi wamefanya vizuri
kwenye orodha za ufungaji mabao msimu huu. Kiungo Clatous Chama wa Simba amefungana kwa mabao manne kileleni na mshambuliaji hatari wa Al Hilal ya Sudan, Makabi Lilepo.

Lakini Fiston Mayele wa Yanga naye anashika nafasi ya pili kwa mabao yake matatu. Paul Aquah wa Rivers United na Aubin Kouame wa Asec Mimosas wanaongoza kwa mabao manne kila mmoja kisha Mayele anafuata.

TIMU PINZANI
Baada ya makundi, timu zinazokutana robo hujipanga kulingana na wanaomaliza nafasi za kwanza kuumana na zilizomaliza kwenye nafasi za pili kwa kuchezeshwa droo. Lakini mpaka sasa haieleweki Simba itakutana na timu zipi tatu za Kundi A, B na D.

Wekundu hao wanamaliza kwenye nafasi ya pili hata baada ya mechi za mwisho kutokana
na uwiano wa pointi za Raja na zao. Timu za kwanza na za pili za Kundi A, B na D hazijafahamika kutokana na uwiano wa pointi, kutotabirika kuwa nani anaenda baina ya timu ya pili na ya kwanza na hata ya tatu pia kulingana na takwimu za kundi husika.

Kundi A haijafahamika ni ipi itamaliza ya kwanza au ya pili baina ya JS Kablyie na Wydad. Kundi B Mamelodi inaongoza lakini Al Hilal ya pili ina kibarua cha mwisho dhidi ya Al Ahly ambao nao wakishinda wanaenda robo.

Kundi D pia haijafahamika kama ni Esperance au Belouizdad itakayomaliza ya kwanza
baada ya mechi za mwisho za makundi. Upande wa Yanga, itafahamika kama inamaliza ya kwanza au ya pili baada ya mechi za mwisho za makundi.

Kundi C, AS FAR inaongoza lakini Future na Pyramids zimefungana kwa pointi nafasi ya pili na ya tatu. Kundi B pia haijafahamika ni Rivers au Asec Mimosas ipi itamaliza ya kwanza.

Kundi A ni kitendawili, USM Alger yenye pointi nane na Saint-Eloi Lupopo na Al Akhdar zenye tano kila moja, bado haijafahamika nani ataungana na Malumo Gallants ambayo imeshafuzu robo kwa pointi zao tisa.

Related Articles

Back to top button