AFCON

Senegal yapewa ubingwa wake

LAUSANNE: SENEGAL imetangazwa kuwa bingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025), baada ya Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) kukubali rufaa yake na kubatilisha uamuzi wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) uliokuwa umeipa Morocco ubingwa huo.

Uamuzi huo umetolewa leo Jumanne, na kuhitimisha mvutano wa kisheria uliodumu kwa miezi kadhaa kuhusu matokeo ya fainali iliyochezwa Januari 18, mwaka huu, mjini Rabat, Morocco.

Senegal ilipata ubingwa kwa bao pekee la muda wa nyongeza kupitia kwa Pape Gueye.

Kabla ya hapo, mchezo huo ulikumbwa na utata baada ya wachezaji wa Senegal kuondoka uwanjani kwa muda wakipinga penalti iliyopewa Morocco, kabla ya kurejea na kuendelea na mchezo.

Machi 17, Kamati ya Rufaa ya CAF ilibatilisha ushindi huo na kuitangaza Morocco mshindi kwa mabao 3-0, ikisema Senegal ilikiuka kanuni za mashindano kwa kuondoka uwanjani kabla ya mchezo kumalizika.

Na Senegal ilipinga uamuzi huo na kuwasilisha rufaa CAS, İkitaka ushindi wake wa uwanjani uheshimiwe.

Baada ya kupitia hoja za pande zote, CAS imekubali rufaa ya Senegal na kuirejeshea ubingwa wake.

Hivyo, ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Morocco unabaki kuwa matokeo yanayotambuliwa ya fainali hiyo.

Uamuzi huo unaifanya Senegal kuandika rekodi ya kutwaa ndoo hiyo mara mbili baada ya kutwaa taji lake la kwanza mwaka 2022.

Related Articles

Back to top button