Muziki

Sammarellah: Washindi wapewe elimu ya usimamizi wa fedha

DAR ES SALAAM: MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Sammarellah, amesema baadhi ya washindi wa shindano la Bongo Star Search (BSS), wanatakiwa kupewa elimu ya fedha.

Akidai kuwa “Wengi wanapopata fedha za ushindi, hubadilika na kuanza kuishi maisha ya kujiona wamefanikiwa zaidi ya walivyo, machawa kibao”.

Kwa mujibu wa kauli yake, baadhi ya washindi hao wanapopata fedha hujikuta wakibadilika kitabia na kusahau misingi iliyowafikisha kwenye mafanikio hayo.

Hali hiyo inaweza kuwafanya wajione wamefika mbali kiasi cha kusahau kuwa muziki ni safari inayohitaji juhudi na uvumilivu.

Sammarellah anaonekana kuonya kuhusu matumizi ya fedha za ushindi bila kuwa na mipango madhubuti ya kuendeleza vipaji vyao.

Anasisitiza kuwa ” “fedha pekee haziwezi kuwa dhamana ya mafanikio ya kudumu katika tasnia ya muziki.

Aidha, kauli yake inaibua swali kuhusu hatima ya washiriki wanaoshinda mashindano ya vipaji lakini baadaye kushindwa kuendeleza majina yao katika muziki.

Je, tatizo ni matumizi ya fedha, kukosa usimamizi mzuri au kushindwa kutumia fursa wanazozipata?

Sammarellah amesema kuna umuhimu wa washindi wa BSS kuwa na nidhamu ya fedha, mikakati ya kimuziki na mipango ya muda mrefu ili fedha za ushindi zisiishie kuwa mafanikio ya muda mfupi, na badala yake ziwe mwanzo wa safari ya mafanikio ya kudumu.

Related Articles

Back to top button