Brand Russell atupwa gerezani miaka 10

LONDON: MCHEKESHAJI, Russell Brand amehukumiwa kifungo cha miaka 10 na miezi 6 gerezani.
Kama inavyofahamika, hukumu hiyo imesomwa baada ya wiki iliyopita, Russell kupatikana na hatia katika shtaka moja la ubakaji na mashtaka matatu ya unyanyasaji wa kijinsia.
Kabla ya kutoa hukumu hiyo, jaji alimkemea vikali Russell kwa namna ya kikatili aliyowatendea waathiriwa watatu, huku akiwabaka na kuwafanyia vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia.
Kuhusu mwathiriwa mmoja, jaji alimshutumu Brand kwa kusema uongo kuhusu kumshika matiti, jambo lililomfanya mwanamke huyo kujisikia vibaya na kupata msongo mkubwa wa kisaikolojia kila alipomwona kwenye televisheni baada ya tukio hilo.
Aidha, baada ya hukumu hiyo, vyanzo mbalimbali vimeuambia Mtandao wa TMZ kuwa mawakili wa Russell wanaandaa nyaraka za kisheria huku wakitafakari uwezekano wa kukata rufaa.
Imeelezwa kuwa mawakili wa Russell walianza kujadili suala la kukata rufaa tangu wiki iliyopita.




