Mastaa

Wolper amfungulia maisha dada yake wa kazi

Sasa ana Benz na nyumba kijijini

DAR ES SALAAM:MSANII wa Bongo Movie na mfanyabiashara, Jacqueline Wolper, amezua gumzo baada ya kueleza namna anavyomjali mfanyakazi wake wa ndani, ambaye amesema anafurahia maisha mazuri kutokana na ajira aliyoipata nyumbani kwake.

Wolper ameeleza kuwa mfanyakazi wake huyo wa ndani anaishi maisha mazuri kiasi cha kuendesha gari aina ya Benz, ambalo limetengwa maalumu kwa ajili ya watoto wake wawili kulitumia wanapokwenda shule.

Mbali na hilo, Wolper amesema mfanyakazi huyo anatumia simu aina ya iPhone, anazungumza lugha ya Kiingereza na kwa sasa anakaribia kukamilisha ujenzi wa nyumba yake kijijini kwao, jambo ambalo amelihusisha na fursa ya ajira aliyoipata kwake.

Akizungumzia zaidi kuhusu mfanyakazi huyo, Wolper amesema ni mtu mwenye tabia nzuri na anayejali familia yake.

Ameeleza kuwa wakati mwingine, anapokuwa hayupo bize, mfanyakazi huyo humpigia simu kwa njia ya video (video call) ili wasali pamoja na watoto.

Wolper amesema kuw pamoja na kumpatia mshahara wake, amekuwa akimsaidia katika mambo mbalimbali yanayolenga kumwezesha kutimiza ndoto zake na kujenga maisha bora.

Aidha, amebainisha kuwa baada ya watoto wake kufikisha umri fulani, mfanyakazi huyo ameonesha nia ya kwenda kusoma masuala ya urembo (make-up), huku Wolper akimshauri kuongeza pia ujuzi wa kutengeneza nywele ili awe na fursa pana zaidi katika sekta ya urembo.

Kupitia mfano huo, Wolper ametoa wito kwa watu waliobahatika kuwa na wafanyakazi wa ndani wachapakazi na wenye tabia njema kutowasahau katika safari zao za kutimiza ndoto.

Amesisitiza kuwa “Pale mtu anapokuwa na uwezo, si vibaya kumsaidia mfanyakazi wake hata katika mambo makubwa kama ujenzi wa nyumba, akieleza kuwa wafanyakazi hao wana mchango mkubwa katika familia, ikiwemo kuitunza nyumba na kuwalea watoto wakati wa majukumu ya kazi.

Wolper ameonyesha kuthamini wafanyakazi wa ndani na umuhimu wa kuwapa nafasi ya kukua, kujifunza na kutimiza ndoto zao kupitia ajira wanazozipata.

Related Articles

Back to top button