EPL

Alonso: Estevao atapata nafasi Chelsea

ENGLAND: KOCHA wa Chelsea, Xabi Alonso, amesisitiza kuwa kiungo mshambuliaji kijana kutoka Brazil, Estevao, atapata nafasi ya kucheza katika kikosi hicho msimu huu licha ya kutotumika katika mchezo wa Kombe la Ligi dhidi ya Liverpool uliochezwa Jumatano katika uwanja wa Anfield.

Mashabiki wa Chelsea walioyesha kutaka kumuona Estevao uwanjani kwa kuimba jina lake mara kadhaa alipokuwa akijiandaa pembeni ya uwanja, wakati timu hizo zikitoshana nguvu kwa sare ya bao 1-1 lonso:kabla Liverpool kushinda kwa mikwaju ya penalti 6-5.

Licha ya mchezo huo kuwa na ushindani mkubwa, Alonso aliamua kutomuingiza nyota huyo mwenye umri wa miaka 19, ambaye amepata dakika 47 pekee za kucheza katika Ligi Kuu England msimu huu, huku akianza michezo miwili ya Kombe la Ligi.

Alonso alieleza kuwa mabadiliko ya wachezaji wakati wa mchezo huo yalichangiwa na hali ya mchezo kuwa ya nguvu kubwa pamoja na changamoto za kiafya zilizowakabili baadhi ya wachezaji wake, akiwemo Moises Caicedo na Malo Gusto.

Hata hivyo, kocha huyo amesema anaelewa kuwa Estevao anatamani kucheza mara kwa mara na kuwa sehemu muhimu ya kikosi, akiahidi kuwa kijana huyo atapata nafasi yake kadiri msimu utakavyoendelea. Alisisitiza kuwa jukumu la kuhakikisha anapata nafasi ni lake kama kocha.

Estevao, aliyesajiliwa na Chelsea kutoka Palmeiras mwaka 2024 kwa ada iliyoripotiwa kuwa pauni milioni 29, alijiunga rasmi na klabu hiyo mwaka uliofuata. Alikuwa amevutia mashabiki baada ya kufunga bao la ushindi dhidi ya Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu England Oktoba mwaka jana.

Chelsea inashika nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi Kuu England na inajiandaa kukutana na Manchester United Jumamosi katika uwanja wake wa nyumbani, Stamford Bridge, huku mashabiki wakisubiri kuona iwapo Estevao atapata nafasi ya kuonesha uwezo wake.

Related Articles

Back to top button