EPL

Maresca aitahadharisha Man City dhidi ya Brighton

ENGLAND: KOCHA wa Manchester City, Enzo Maresca, amesema kikosi chake kinapaswa kujiandaa kwa mchezo mwingine mgumu dhidi ya Brighton, watakapokutana tena Jumamosi(leo Oktoba 31,2026) katika Ligi Kuu England, siku chache baada ya kukutana katika Kombe la Ligi (Carabao).

City ilifanikiwa kuiondosha Brighton katika hatua ya Kombe la Ligi Jumatano, baada ya timu hizo kutoka sare ya mabao 2-2 ndani ya dakika 90 kabla wenyeji kushinda kwa mikwaju ya penalti na kufuzu robo fainali.

Mchezo huo ulionesha ushindani mkubwa, huku Brighton ikitangulia mara mbili kupitia Malick Yalcouye na Georginio Rutter, kabla ya Mateo Kovacic na Vitor Reis kuisawazishia City na kupeleka mchezo kwenye mikwaju ya penalti.

Maresca amesema Brighton iko katika kiwango kizuri kwa sasa, ikionyesha uwezo mkubwa wa kushambulia na kufunga mabao mengi. Ameonya kuwa City haitarajii mchezo mwepesi, hasa kutokana na mfumo wa wapinzani wao wa kucheza kwa presha na kuwafuata wapinzani mmoja mmoja.

Mchezo wa Jumamosi unatarajiwa kuwa na ushindani zaidi, kwani makocha wote wawili wanatarajiwa kutumia vikosi vyao imara baada ya kufanya jumla ya mabadiliko 16 katika mchezo wa Kombe la Ligi. Kwa sasa City inaongoza ligi ikiwa sare ya pointi na Arsenal, huku Brighton ikiwa nafasi ya tatu kwa tofauti ya pointi tano.

Wakati huo huo, Manchester City inaendelea kukabiliwa na kivuli cha tuhuma zaidi ya 100 za kukiuka kanuni za kifedha za Ligi Kuu England, ambazo ilikutwa na hatia mwezi uliopita. Klabu hiyo imekata rufaa na imekanusha makosa hayo, huku adhabu yoyote dhidi yake ikiwa bado haijatangazwa.

Licha ya changamoto hizo, Maresca amesema anaendelea kuelekeza nguvu zake katika mafanikio ya uwanjani.

City pia imepangwa kukutana na Bradford, inayoshiriki daraja la tatu nchini England, katika robo fainali ya Kombe la Ligi, huku kocha huyo akisisitiza kuwa malengo ya klabu hiyo ni kuendelea kupigania mataji katika kila mashindano.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button